Search This Blog

Tuesday, February 2, 2021

Bulaya atinga Bungeni leo, ataja anachokitaka

 


Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ester Bulaya, leo ameingia Bungeni pamoja na baadhi ya wabunge wenzake wa chama hicho na kueleza kuwa suala la kutokamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara limekuwa ni tatizo sugu na kuhoji ni lini barabara ya Kisorya, Bunda itakamilika.


Ni katika Kikao cha Kwanza cha mkutano wa pili wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ndipo alipouliza swali hilo kwa Wizara ya Ujenzi, huku akieleza kuwa mchakato wa ujenzi wa barabara umechukua takribani miaka 15 sasa.


"Uchelewashwaji wa ukamilishwaji wa miradi ya barabara limekuwa ni tatizo sugu, hapa ninapozungumza ujenzi wa barabara wa kutoka Kisorya, Bunda, ahadi na uanzaji wake umechukua takribani miaka 15, sasa nataka kujua ni lini hiyo barabara itakamilika kwa sababu ikikamilika inaunganisha na barabara ya Serengeti na imekuwa kilio kikubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara", amesema Mbunge Ester Bulaya.


Ikumbukwe kuwa Ester Bulaya na wenzake 18, walikwishafukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA, baada ya wao kwenda kula kiapo cha ubunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama chao, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni wasaliti.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...