Search This Blog

Tuesday, February 16, 2021

Hii hapa ratiba leo ya michezo ya ligi kuu


 LEO Februari 16, Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni mzunguko wa pili ambapo mechi mbili kali zitapigwa viwanja viwili tofauti.

Gwambina iliyo nafasi ya 15 na pointi 20 baada ya kucheza mechi 18 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya tano na pointi 28 na imecheza mechi 19.Utakuwa Uwanja wa Gwambina Complex.

KMC iliyo nafasi ya 6 na pointi 25 baada ya kucheza jumla ya mechi 19 inakutana na Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 15 baada ya kucheza jumla ya mechi 19. Utakuwa ni Uwanja wa Uhuru.

Kinara wa Ligi Kuu Bara Tanzania ni Yanga ana pointi 45 baada ya kucheza jumla ya mechi 19.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...