Mwezi Disemba Bunge la DRC lilimg'oa madarakani Spika Jeanine Mabunda, ambaye ni mshirika wa Joseph KabilaImage caption: Mwezi Disemba Bunge la DRC lilimg'oa madarakani Spika Jeanine Mabunda, ambaye ni mshirika wa Joseph Kabila
Wabunge wa bunge dogo la DRC wanatarajiwa kumchagua Spika mpya leo, huku Rais Felix Tshisekedi akikusanya nguvu chini ya muungano wake mpya unaoitwa –Muungano mtakatifu.
Hii inafuatia kuondolewa kwa Spika Jeanine Mabunda, ambaye ni mshirika wa rais wa zamani Joseph Kabila, ambaye aliondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye mwezi Disemba kufuatia tuhuma za ufisadi.
Jana zaidi ya maseneta 60 waliwasilisha ombi la kutimuliwa madarakani kwa Spika wa bunge la Seneti Alexis Thambwe Mwamba, kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali ya umma.
Mwamba, mbaye pia ni mshirika wa Bw Kabila, anashutumiwa kuchukua zaidi ya dola milioni 3 za kimareani kwa niaba ya Seneti. Amekana tuhuma hizo.
Wiki iliyopita Waziri Mkuu Sylivestre Illunga alijiuzulu baada ya kura ya kutokuwa na imani naye kupigwa dhidi yake.
Tshisekedi amekuwa akiwatimua washirika wa mtangulizi wake tangu alipovunja muungano mwezi Disemba mwaka jana kufuatia kuongezeka kwa tofauti kuhusiana na mageuzi ya usalama, mahakama, tume ya uchaguzi na mashirika mbali mbali ya taifa.

No comments:
Post a Comment