Balozi wa Marekani mjini Ankara David Satterfield, amesema kuwa Uturuki ni mshirika muhimu wa NATO, na kwamba wanapaswa kutilia mkazo suala la uhusiano wao.
Balozi huyo wa Marekani mjini Ankara David Satterfield alitoa maelezo hayo alipozungumza na waandishi wa habari.
Akisisitiza kwamba uhusiano wa nchi mbili utapewa umuhimu wakati wa utawala wa Rais mpya wa Marekani Joe Biden, Satterfield alisema,
"Kwa upande wetu, Uturuki ni mshirika wa thamani wa NATO na tunaona umuhimu wa uhusiano wetu na vipimo vyake vyote."
Balozi Satterfield pia alibainisha kuwa ndani ya miezi michache iliyopita, nchi ya Uturuki iliongezeka kuwa na wawekezaji wa kigeni, kuboresha thamani ya lira ya Uturuki, jambo ambalo linatia moyo.
Balozi huyo aliongeza kusema kuwa Marekani daima imekuwa na imani na nguvu ya kimsingi kwa uchumi wa Uturuki.

No comments:
Post a Comment