Search This Blog

Sunday, February 21, 2021

Alexei Navalny apigwa faini kwa "kumkashifu" mkongwe wa vita vya pili vya dunia nchini Urusi

 


Mahakma nchini Urusi imetoa uamuzi wa kesi ya pili iliyokuwa ikimkabili kiongozi wa upinzani Alexei Navalny. 


Navalny, alipatikana na hatia ya kumkashifu mkongwe mmoja aliyeshiriki kwenye wa vita vya pili vya dunia na hivyo ametakiwa kulipa faini ya karibu Euro 9,500. 


Kabla ya hapo, mahakama ilitupilia mbali rufaa ya kesi yake nyingine aliyowasilisha kupinga umauzi wa kumfunga jela miaka mitatu kwa kosa la kukiuka dhamana. 


Wafuasi wake wanadai kuwa mashtaka yote mawili ni njama ya kisiasa ambapo serikali inataka kuunyamazisha upinzani dhidi ya rais wa Urusi Vladimir Putin.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...