Search This Blog

Friday, January 29, 2021

Wataalam wa WHO waanza uchunguzi wa virusi vya corona Wuhan


Wataalam wa Shirika la Afya Duniani, WHO leo wameitembelea hospitali moja ya Wuhan na kuanza uchunguzi kuhusu chimbuko la virusi vya corona. 

Wataalam hao watalichunguza pia soko moja la chakula linalodaiwa kuwa ndipo virusi hivyo vilipoanzia.

 Uchunguzi huo wa WHO umecheleweshwa na kumekuwa na hofu kuhusiana na kupata ushahidi mwaka mmoja baada ya virusi hivyo kuibuka katika mji huo wa China

. Timu hiyo ilikutana na maafisa wa China na wakaondoka katika hoteli yao mjini Wuhan. Maeneo yote yatakayotembelewa na wataalam hao bado hayajajulikana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...