Waliofukuzwa uanachama katika chama cha upinzani cha Chadema ni miongoni mwa walioteuliwa katika kamati za bunge.
Akifanya uteuzi huo wa wajumbe wa kamati za kudumu za bunge la 17, Spika wa Bunge Job Ndugai amejumuisha waliofutwa uanachama katika chama cha Chadema.
Miongoni mwa wabunge waliotajwa ni Naghenjwa Kaboyoka aliyetetea uenyekiti wa kamati ya hesabu za serikali (PAC) na Grace Tendega aliyeshinda uenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa (LAAC), gazeti la Mwanachi limesema.
Wabunge hao ni miongoni mwa wale waliokwenda bungeni Dodoma na kuapishwa bila idhini ya chama.
Kulingana na kanuni za bunge, kamati hizo zinastahili kuongozwa na wabunge wa upinzani.
Hata hivyo makamu waliochaguliwa katika kamati hizo za LAAC na PAC ni wa CCM, Seleman Zedi Mbunge wa Bukene na Mbunge wa jimbo la Vwawa (CCM), Japhet Hasunga mtawalia.
Hata hivyo nafasi nyingi zimewaendea wabunge wa CCM.

No comments:
Post a Comment