Search This Blog

Sunday, January 24, 2021

Walimu wapya 68 Masasi wapatiwa magodoro


Na Hamisi Nasri, Masasi.

WATUMISHI wapya 68 ambao ni walimu waliokuja kuripoti na kupangiwa vituo vya kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamepatiwa magodoro 68 yenye tahamani ya sh.6,080,000 milioni kwa ajili ya kwenda kuanzia maisha wakati wakitekeleza majukumu yao.

Walimu hao walipatiwa magodoro hayo jana mjini Masasi katika hafla fupi iliyoandaliwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya kuwapatia vifaa hivyo,tukio ambalo liliudhuliwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Ryoba Magabe pamoja na mkuu na wilaya ya Masasi, Selemani Mzee kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mtwara,Gelasius Byakanwa   

Akizungumza kabla ya kuwakabidhi magodoro hayo kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa halmashauri imepokea jumla ya watumishi wapya 68 ambao ni walimu wapya kwa ajili ya kufanya kazi katika halmashauri hiyo. 

Alisema walimu hao tayari halmashauri imeshawapangia vituo vyao vya kazi na kwamba imeshaweka mzingira yote vizuri ambayo watakuwa wakifanyia kazi. 

Magabe alisema mwezi Disemba halmashauri ilipokea watumishi hao ikiwa ni ajira mpya ilitolewa na hivi karibu na serikali na kwamba halmashauri imeshukuru kwa kupata watumishi hao. 

“Halmashauri imeamua kuwapatia magodoro haya watumishi hawa ambayo thamani yake ni sh.6,080,000 ili wakaanze vema maisha yao ya kiutumishi wakiwa na mazingira mazuri…tunaipongeza serikali kwa kutupatia watumishi hawa,”alisema Magabe   

Akizungumza na watumishi hao, mkuu wa wilaya ya Masasi, Selemani Mzee aliwaasa walimu hao kwenda kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za utumishi wa umma sambamba na kufanya kazi kwa bidii. 

Aidha,Mzee alisema watumishi hao watumie fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi kwa kujiunua kiuchumi ikiwemo kumiliki ardhi kwa ajili ya kujenga makazi, kilimo na shughuli zingine za kiuchumi.  

Alisema kusini kuna fursa nyingi za kiuchumi kama vile mashamba ya korosho na ufuta hivyo walimu hao wazitumie fursa hizo pia kujiongezea kipato wakati wakiendelea na majukumu yao.  

Wakizungumza na Muungwana Blog baadhi ya walimu hao kwa niaba ya watumishi wenzao wameipongeza halmashauri kwa kuwapatia magodoro hayo na kwamba watafanya kazi kwa kuzingatia miongozo ya utumishi wa umma.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...