Search This Blog

Sunday, January 3, 2021

Vifo vya corona vyaongezeka Ujerumani

 


Taasisi ya Ujerumani ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Robert Koch imesema nusu ya vifo vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani vilitokea mnamo mwezi Desemba. 

Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi hiyo watu wapatao 16,718 walikufa kati ya mwezi Desemba hadi Januari mosi. 

Kwa jumla watu 33,071 wameshakufa nchini Ujerumani tangu kulipuka kwa maambukizi ya virusi vya corona mwaka uliopita. Idadi ya walioambukizwa ilifikia 1,719,737 hadi mwezi uliopita. 

Madaktari wametoa mwito wa kuchukuliwa hatua kali zaidi ili kupunguza maambukizi. Mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani wanatarajiwa kukutana ili kuamua iwapo vizuizi vilivyowekwa hadi tarehe 10 Januari vitaendelezwa. 

Wakati huo huo, Ujerumani pamoja na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya zilianza kutoa chanjo dhidi ya corona mwezi Desemba na hadi mwishoni mwa mwezi huo watu 131,626 walikuwa wameshapatiwa chanjo hizo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...