Saudi Arabia imesema itaondoa marufuku ya muda iliyoweka kwa ndege za abiria kutoka Uingereza na Afrika Kusini hii leo Jumapili.
Hatua hiyo ilichukuliwa wiki mbili wiki zilizopita kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya aina mpya ya homa ya Covid-19 iliyozuka nchini Uingereza.
Shirika la habari la Saudi Arabia -SPA limeripoti juu ya kuondolewa marufuku hiyo limesema wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imetoa mwongozo kwamba watu wasio raia wa nchi hiyo wanaotoka Uingereza na Afrika Kusini watalazimika kwanza kukaa siku 14 nje ya nchi hizo kabla ya kusafiri kwenda Saudi Arabia na ni lazima kuonyesha vyeti kuwa hawana maambukizi ya corona mara tu wanapofika.

No comments:
Post a Comment