Urusi inafanya mazungumzo na maafisa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa ajili ya kutumia anga yake kusaidia kudhibiti hali kwa matatizo ya kiusalama yanayoongezeka nchi hiyo.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya kitaifa, iliarifiwa kwamba maafisa wa Urusi walikutana na maafisa wa CAR kwa mazungumzo ya kuruhusu ndege za jeshi la Urusi kutoa msaada wa ulinzi wa anga kwa nchi hiyo na kudhibiti hali ya usalama dhidi ya waasi.
Serikali ya CAR bado haijatoa taarifa rasmi juu ya suala hilo.
Katika nchi hiyo ambayo karibia asilimia 80 inadhibitiwa na vikundi vyenye silaha vya waasi na vilivyokuwa chini ya mwavuli wa muungano wa chama cha Patriots for Change (CPC), kulianzisha mashambulizi ya kuteka mji mkuu wa Bangui.
Waziri wa Mambo ya Nje wa CAR Sylvie Temon aliomba msaada kwa Urusi na Rwanda wakati wa mchakato wa uchaguzi nchini humo mwezi uliopita. Rwanda na Urusi zilijibu vyema ombi la CAR na kutuma mamia ya wanajeshi nchini. Mamlaka ya Urusi ilibaini kuwa, mbali na maafisa 14 wa Urusi kutoka Vikosi vya Udhibiti vya Umoja wa Mataifa (MINUSCA), idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi walipelekwa nchini kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo kufuatia ombi la maafisa.

No comments:
Post a Comment