Serikali ya Shirikisho la Ujerumani pamoja na za majimbo zinapanga kutangaza amri ya kutotembea nje usiku ili kuzuia maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha corona. Haya ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vikinukuu taarifa kutoka Ofisi ya Kansela.
Bado kuna mjadala wa ni kuanzia lini amri kama hiyo inapaswa kutumiwa na kama inapaswa kutekelezwa kutokana na tukio fulani.
Kansela Angela Merkel atafanya mkutano na Mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani kesho kujadili uwezekano wa kuimarisha hatua kali za kudhibiti ugonjwa wa COVID-19.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amesema watu waliopata chanjo ya corona wanapaswa kuruhusiwa kwenda migahawani na kumbi za sinema mapema kabla ya wengine.
Kauli hiyo inatofautiana na ya mawaziri wengine wanaopinga uhuru maalum kwa waliopewa chanjo.

No comments:
Post a Comment