Search This Blog

Monday, January 18, 2021

Navalny akamatwa baada ya kutua Moscow


Mkosaji wa rais wa Urusi Vradimir Putin , Alexei Navalny amekamatwa baada ya kurejea mjini Moscow kwa ndege akitokea Ujerumani, miezi mitano baada ya kushambuliwa kwa sumu ya neva ambayo nusura imuue.

Mwanaharakati huyo, mwenye umri wa miaka 44, alichukuliwa na polisi katika kitengo cha udhibiti wa pasipoti katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo.

Maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika katika viwanja tofauti vya ndege vya mjini Moscow kuipokea ndege yake iliyokuwa ikijtokea mjini Berlin, lakini ndege yake ilielekezwa kwenye uwanja tofauti.

Bw Navalny anazilaumu mamlaka za Urusi kwa jaribio la kumuua mwaka jana. Utawala wa Kremlin unakana kuhusika na shambulio hilo la sumu.

Madai ya mwanasiasa huyo wa upinzani hata hivyo yamekua yakiungwa mkono na ripoti za waandishi wa habari wa taarifa za uchunguzi.

Kukamatwa kwa Bw Navalny kumelaaniwa na Muungano wa Ulaya, Ufaransa na Italia , ambao wametoa wito aachiliwe mara moja.

Mshauri ajaye wa masuala ya usalama wa taifa wa Rais mteule wa Marekani Joe Biden pia ameunga mkono wito huo "Shambulio la Kremlin dhidi ya Bw Mr Navalny si ukiukaji tu wa haki za binadamu, lakini pia ni unyanyasaji kwa watu wa Urusi ambao wanataka sauti yao isikike ," Jake Sullivan alisema.

Wakati Bw Navalny alipopewa sumu mwezi Agosti mwaka jana na kuzimia katika safari ya ndege ya kimataifa, alisafirishwa hadi nchini Ujerumani kwa ajili ya kupata huduma za matibabu za dharura. Alipokuwa akiendelea kupona , alisema anaazimia kurejea Urusi.

Jumapili alitimiza ahadi hiyo, akapanda ndege ya Pobeda Airlines, licha ya kwamba alionywa kuwa anakabiliwa na hatari ya kukamatwa mara tu ndege yake itakapotua.

Ndege yake ilikuwa imejaa waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na Andrey Kozenko mwandishi wa BBC wa Idhaa ya Kirusi. Muda mfupi kabla ya ndege kutua, rubani alitangaza kuwa ''kutokana na sababu za kiufundi'', ndege yao haitatua katika uwanja wa ndege wa Vnukovo na badala yake itatua katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo, jambo lililosababisha wasiwasi miongoni mwa abiria.

"Ninajua hilo . Siogopi lolote," Bw Navalny aliwaambia waandishi wa habari na wafuasi wake alipowasili, dakika chache tu kabda ya kukamatwa . "Tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu ?" aliwauliza walinzi wa mpakani.

Alimbusu mke wake Yulia - ambaye alikuwa amesafiri na yeye kutoka Ujerumani-baada ya maafisa wa polisi kuonya kuwa wangetumia nguvu iwapo angepinga maagizo ya kuambatana nao. Licha ya kuwaomba , wakili wa wa Bw Navalny' hakuruhusiwa kuambatana naye.

Mwanaharakati huyo kwa sasa nashikiwa katika kituo cha polisi mjini Moscow.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...