Watu wapatao 16,718 wameripotiwa kufariki kutokana na virusi hivyo kati ya Desemba 2 na Januari mosi, kulingana na Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani ya Robert Koch. Zaidi ya nusu ya vifo vyote vilivyotokana na COVID-19 nchini Ujerumani vilitokea mwezi Desemba.
Kwa jumla, watu 33,071 walikufa Ujerumani kutokana na ugonjwa huo mwaka uliopita wa 2020.
Susanne Johna, mkuu wa umoja wa madaktari amehimiza leo kuongezwe muda wa kuendelea na masharti yaliyowekwa kupambana na kuenea kwa virusi hivyo, ambao unatarajiwa kumalizika Januari 10. Mawaziri watakutana Jumanne ijayo kujadili suala hilo.
Desemba ulikuwa mwezi mbaya zaidi nchini Ujerumani katika janga la virusi vya corona kutokana na kuongezeka mara tatu kwa idadi ya vifo tangu Novemba.

No comments:
Post a Comment