Search This Blog

Thursday, January 28, 2021

Tetesi za soka kimataifa

 


Paris St-Germain 'imekosa heshima' katika kusaka saini ya kiungo mchezeshaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kulingana na rais wa Barcelona Joan Laporta, ambaye ametishia kuiripoti klabu hiyo ya Ligue 1 kwa Fifa. (Goal)

West Ham huenda ikasitisha hamu yao ya mshambuliaji mpya katika dirisha la uhamisho iwapo itafanikiwa kumsajilki kwa mkopo winga wa Man United na England Jesse Lingard, 28. (The Athletic - subscription required)

Kiungo wa kati wa Ufaransa France Paul Pogba, 27, anasema kwamba atafanya mazungumzo na Man United mwisho wa msimu huu ili kutoa suluhu ya kudumu kuhusu hatma yake katika uwanja wa Old Trafford.. (Mail)

West Brom wamekubali kumsajili mshambuliaji wa Galatasaray na Senegal Mbaye Diagne, 29, kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia. (Express & Star)

Kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli anafikiria kujiunga na Paris St-Germain, lakini mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy hataki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuondoka. (ESPN)

Iwapo Spurs itamuachilia Alli kuondoka , huenda ikamsajili kiungo wa kati wa klabu ya Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka ,23 raia wa Ujerumani Florian Neuhaus. (Mirror)

Tottenham inamchunguza beki wa kati wa Napoli na Serbia Nikola Maksimovic, 29. (Sun)

Manchester City wamekubali kumuuza beki wa Uhispania Eric Garcia, 20,kwa Barcelona na mchezaji huyo atalazimika kucheza bila malipo kwa miezi sita ili kuweza kuhamia katika klabu hiyo anasema rais Victor Font. (Goal)

Hatma ya beki wa Kushoto wa Marekani DeAndre Yedlin katika klabu ya Newcastle huenda itategemea ufanisi wa klabu hiyo katika kuwasajili wachezaji kwa mkopo katika siku za mwisho za dirisha la uhamisho. (Newcastle Chronicle)

Galatasaray imewasilisha ombi la kutaka kumsajili Yedlin mwenye umri wa miaka 27. (ESPN)

Thomas Tuchel atashirikiana na wasaidizi wake wa kiufundi katika klabu ya Chelsea huku naibu kocha Arno Michels na kocha Zsolt Low wakitarajiwa kujiunga naye katika klabu ya Stamford Bridge. (London Evening Standard)

Beki Lukasz Bejger, 19, anasema kwamba alilazimika kuondoka Manchester United na kurudi kuichezea klabu ya nyumbani ya Slask Wroclaw nchini Poland ili kupata uzoefu katika soka ya watu wazima..(Manchester Evening News)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...