Mfanyabiashara wa Muisraeli anashitakiwa mjini Geneva Jumatatu kwa mashitaka ya ufisadi unaohusiana na haki za uchimbaji wa madini ya chuma nchini Guinea.
Beny Steinmetz, ambaye tayari alikwisha hukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na mahakama ya Romania bila kwa utakatishaji wa fedha bila kuwepo mahakamani, atafika mahakamani mwenyewe mjini Geneva.
Amekuwa akikana madai yote ya ufisadi dhidi yake.
Waendesha mashitaka wa Uswiss walisema alilipa hongo ya mamilioni ya dola , baadhi kupitia akaunti za benki za Uswiss , ili kupata haki ya kuchimba madini ya chuma ya Guinea katika machimbo ambayo hayajawahi kuchimbwa duniani.
Hongo hizo – kwa maafisa wa umma wa Guinea –zilidaiwa kulipwa kwa usaidizi wamjane wa rais wa zamani wa Guinea Mamadou Toure, Lansana Conte.
Amekuwa akielezewa kama shahidi nyota wa uendesha mashitaka- lakini huenda asiwepo mahakamani.
Kwa sasa Bi Lansana Conte anaishi nchini Marekani.
Beny Steinmetz atafika mahakamani na anatarajiwa kukanusha tuhuma zote. Iwapo atapatikana na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela.

No comments:
Post a Comment