Search This Blog

Saturday, January 30, 2021

Taasisi zahimizwa kutenga mda kufanya mazoezi ya pamoja na watumishi wao


Na Ezekiel Mtonyole - Dodoma.

Taasisi za Umma na binafsi zimehimizwa kujenga utaratibu wa kuwakusanya watumishi wao na kufanya mazoezi ya pamoja ili kujenga uhusiano mzuri baina yao ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya zao.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt Allan Kijazi mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya pamoja ya watumishi wa Wizara hiyo kushirikiana na baadhi ya klabu za mazoezi za Jiji la Dodoma.

Amesema ni vyema taasisi zikajenga utaratibu wa kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja ili kujenga muamuko kwa watumishi kufanya mazoezi  kuimarisha afya zao.

"Mazoezi ni mazuri kwa afya lakini muamuko ni mdogo katika kufanya mazoezi lakini taasisi zikiwazinakutana na kufanya mazoezi kwa pamoja watu watapenda kufanya mazoezi wao binafsi kuimarisha afya na kuepuka magonjwa" amesema.

Amesema mazoezi hayo ni mara ya kwanza lakini yatakuwa ni endelevu katika kujenga uhusiano baina ya watumishi na kuimarisha afya zao pia wataboresha utendaji kazi wao wa kila siku.

Amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kufanya mazoezi na wasiishie siku hiyo, pia ametaka watumishi hao kujiunga katika klabu za mazoezi ili kuimarisha afya zao waweze kuepuka magonjwa yatokanayo na kutofanya mazoezi.

Aidha amezipongeza klabu za mazoezi za Dodoma fitness center na Muungano vya Jijini Dodoma kwa kushirikiana na watumishi wa Wizara katika kufanya mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika uwanja Jamhuri jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu za mazoezi Dodoma kutoka klabu ya Dodoma fitness center Mugisha Mujungu amesema kwa Dodoma kuna vilabu sita(6) vya kufanya mazoezi na kuwahimiza watumishi wa Wizara ya Maliasili na utalii kujiunga ili kufanya mazoezi kuboresha afya.

"Kuna klabu sita zilizosajiliwa kwa hapa Dodoma ni vema mkajiunga na klabu hizi ili kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuepukika kwa kufanya mazoezi" amesema Mujungu



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...