Search This Blog

Friday, January 29, 2021

Sherehe ya siku ya kuzaliwa yamtia mashakani Cristiano Ronaldo


Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo anachunguzwa na maafisa wa polisi wa Itali kuhusu safari aliokwenda ili kusherehekea siku ya kuzaliwa na mpenzi wake.

Anatuhumiwa kwa kuvunja masharti ya Covid -19 kwa kusafiri kati ya jimbo la Piedmont na Valle d'Aosta.

Picha zilizochapishwa na baadaye kuondolewa mtandaoni zinawaonesha wawili hao wakiwa katika hoteli moja siku ambayo Georgina Rodriguez alisherehekea kua na umri wa miaka 27.

Italy imeshuhudia mamia ya vifo na maelfu ya maambukizi mapya kila siku.

Taifa hilo liliathiriwa vibaya mapema wakati wa mlipuko huo mwaka uliopoita na sasa liko katika mzozo wa ksiasa baada ya kushindwa kupunguza idadi maambukizi katika wimbi la pili la maradhi hayo.

Maafisa wa polsi wa Valle d'Aosta wanasema kwamba wanawachunguza wapenzi hao kuhusu safari hiyo ya mgahawa wa Courmayeur ski

Chini ya sheria zilizopo nchini Itali, safari kati ya maeneo yenye maambukizi ya Corona zimepigwa marufuku isipokuwa iwapo ni ziara ya kikazi ama kwenda nyumbani

Ripoti nchini Itali zinadai kwamba wawili hao walisafiri siku ya Jumanne na kusalia katika mgahawa huo usiku kucha kabla ya kurudi Turin, nyumbani kwa klabu ya Serie A Juventus siku ya Jumatano.

Rodriguez, ambaye ni mwanamitindo , baadaye alichapisha picha ya yeye na Ronaldo wakisherehekea nyumbani kwao na familia



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...