Search This Blog

Wednesday, January 27, 2021

Raia wa Rwanda wavunja masharti ya Covid-19 kusheherekea ushindi

 


Watu walimiminika katika barabara za Kigali siku ya Jumanne baada ya timu ya taifa la nchi hiyo kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN , ingawa kuliwekwa marufuku ya wiki mbili ya kutotoka nje jijini humo.

Picha za mamia ya watu wakiimba kwa furaha na kukimbia bila barakoa wala kufuata masharti ya kutokaribiana, zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wakazi walituma ujumbe wa Twitter wakiomba polisi wa nchi hiyo kufunguliwa milango ya uwanja huo wa Nyamirambo wakisema ‘lazima washerehekee ushindi wa Amavubi kwa ‘gharama yoyote’.

''Sikukumbuka corona, haikuwa ikiwezekana kubaki nyumbani, kelele za vuvuzela zilisikika kila mahali mpaka baada ya saa sita usiku'' , alisema Elie Karinganire mkazi wa Kigali alipozungumza na BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

Rwanda ilichapa Togo magoli matatu kwa mawili, na kufuzu katika hatua ya mtoano katika michuano inayoendelea nchini Cameroon.

Picha ziliwaonesha polisi wakiingilia kati katika baadhi ya maeneo na kuwaamuru warejee majumbani mwao. Katika hatua ya robo fainali siku ya Jumapili Rwanda itakabiliana na Guinea au Zambia, mshindi wa kundi D atajulikana baada ya mchezo wa leo.

Sherehe za mjini Kigali zimefanyika baada tu ya Wizara ya Afya ya Rwanda kutangaza kuwepo kwa wagonjwa 574 wa Covid-19, idadi kubwa kuwahi kurekodiwa tangu alipobainika mtu wa kwanza mwezi Machi mwaka jana.






No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...