Search This Blog

Wednesday, January 27, 2021

Ethiopia kuondoa wanajeshi mpakani mwa Sudan


Ethiopia inataka iondoe wanajeshi wake kutoka nchi ya Sudan ambayo ilidai kuvamiwa ardhi za mpaka wake.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia Dina Mufti, alizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa wiki na kusema kwamba nchi yake imeazimia kutatua suala la mipaka kwa amani.

Akitoa wito kwa Sudan kwamba watazingatia hali hiyo kabla ya Desemba 2020 na kuondoa wanajeshi kutoka eneo lenye mgogoro la Fashka, Mufti alisema kuwa nchi hizo mbili zina kamati za ufundi na siasa na zinazohitaji kutatua mzozo kwa njia ya mazungumzo.

Mvutano kati ya Sudan na Ethiopia uliokuwepo kwa miaka mingi kutokana na madai ya "ukiukaji wa mipaka", umeongezeka kufuatia ujenzi wa kambi za majeshi ya nchi hizo mbili kwenye maeneo ya karibu na Fashka katika miezi ya hivi karibuni.

Mnamo Desemba 2020, Khartoum ilitangaza kwamba imechukua tena ardhi za Sudan zilizokuwa zikidhibitiwa na "wanamgambo wa Ethiopia" kwa takriban miaka 20 na kuhalalishwa katika makubaliano ya kimataifa.

lilishutumu jeshi la Sudan kwa kuchukua ardhi yake.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdullah Hamduk alisema katika mkutano wake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ulioanyika mnamo Januari 21 kwamba vikosi vya usalama vinafanya kazi ndani ya eneo lao na hawataki vita yeyote.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...