Search This Blog

Monday, January 4, 2021

Mwakamo aipigia chapuo Mlandizi Queen's

 ojasirasa mngindo <ojasirasamngindo@gmail.com>

AttachmentsSun, 3 Jan, 14:46 (20 hours ago)

to me

Makurunge wasafisha eneo la kujenga Sekondari


Na Omary Mngindo, Makurunge

Jan 3


WAKAZI wa Vitongoji vya Mkwajuni, Gezaulole, Mtoni, Kitame, Kifude na Kibaoni Kata ya Makurunge Jimbo la Bagamoyo Pwani, wameanza kusafisha eneo litalojengwa shule ya sekondari ya Kata hiyo.


Usafi huo ulioanzia kwa kutumia greda walilolikodi kwa shilingi milioni moja na laki nane kwa siku mbili, inatokana na michango iliyotolewa na viongozi wa serikali kwa niaba ya wananchi wa maeneo yao, hatua inayolenga kuwaondolea adha wanafunzi.


Wakizungumza na Waandishi wa habari eneo la tukio, Diwani wa Kata Hamisi Mbonde alisema hatua hiyo inalenga kuwaondolea adha wanafunzi wanaosafiri mpaka Fukayosi au Kata ya Magomeni kupata elimu, hali inayosababisha usumbufu mkubwa.


"Kwa kila siku mzazi au mlezi amalazimika kutumia zaidi ya shilingi elfu mbili kwa ajili ya nauli ya wanafunzi kwenda Fukayosi na kurudi, hali ambayo ni mzigo mkubwa ukizingatia kipato chao hakikidhi gharama hiyo," alisema Mbonde.


Aliongeza kwamba baada ya usafi huo wanataraji kuwajulisha wananchi wote katani hao kufika tayari kuanza kuchimba msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hiyo, inayitaraji kuanza kupokea wanafunzi mwezi wa pili mwaka huu.


"Harakati hizi zinaungwa mkono kwa asilimia kubwa na Mbunge wetu Muharani Mkenge, ambaye alipokuwa kwenye ziara ya kushukuru hivi karibuni aliutaka uongozi wa Kata kumjulisha siku ya kuanza kuvhimba msingi ili nae aweze kuhudhulia," alisema Mbonde.


Alisema kwamba wanayo matofari zaidi ya elfu sita, nondo na vifaa vinavyohusiana na ujenzi, na kuwa matarajio yao ni kukimbizana na agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa la kuwataka viongozi kujenga shule mpya au vyumba vya kutosha ili kuwapokea wanafunzi wote wataofaulu.


Kwa upande wao Hamisi Mwanamkuta Ofisa Elimu Kata, Juma Ngwambi Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mkwajuni, Amani Mdoe Mwenyekiti Jumuia ya Wazazi Kata na Hussein Mwinyimvua Katibu wa Vitongoji cha Gezaule walisema kwamba wana-Makurunge wameupokea kwa moyo mmoja ujenzi huo.


"Wana-Makurunge wamehamasika sana kwani kwa miaka mingi vijana wetu walikuwa wanakwenda umbali mrefu kufuata masomo, wazazi walikuwa wanalazimika kutumia zaidi ya shilingi elfu mbili kwa ajili ya nauli na hela ya kula," alisema Mwinyimvua.


MWISHO.


Mwakamo aipigia chapuo Mlandizi Queen's


Na Omary Mngindo, Mlandizi 

 MBUNGE wa Jimbo la  Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo amewaomba wana-Kibaha Vijijini na Vitongoji vya jirani kujiyokeza kuisaidia timu ya soka ya Mlandizi Queen's ili iendelee kufanya vizuri.

Mwakamo alitoa rai hiyo Jan Mosi aliposhiriki hafla ya chakula cha pamoja katika kituo cha kulelea watoto wenye mazingira hatarishi cha Masjid Nour cha Mlandizi, iliyoandaliwa na ofisi yake akishirikiana na wadau iliyowashirikisha wachezaji na viongozi wa timu hiyo, ambapo alisema timu inapashwa kusaidiwa.

"Hii timu kwanza ina jina letu la Mlandizi tunapaswa kujivunia, usitoshe imeweka historia kubwa katika soka la Wanawake hapa nchini, kwani ni timu ya kwanza kuutwaa ubingwa wa Ligi hiyo iliyoshirikisha vilabu mbalimbali vikiwemo vya Yanga na Simba," alisema Mwakamo

Aliongeza kuwa pamoja na juhudi hizo lakini inapata ushirikiano mdogo kutoka kwa wana-Mlandizi, hivyo amewaomba kuuthamini mchango huo kutoka kwa vijana hao, ambao wachezaji wake kadhaa wanaunda timu ya Taifa ya Wanawake (Taifa Queen's).

"Hii nafasi tuliyonayo inapaswa tuiangalie kwa macho mawili mawili, kuna mikoa inatamani kuwa na fursa kama hii lakini hawana, niwaombe wana-Kibaha wenzangu tuichukulie timu hii kama kioo cha Mlandizi na Jimbo zima la Kibaha Vijijini," alisema Mbunge huyo.

Aliongeza kuwa kutokana na thamani hiyo anawaomba wana-Mlandizi kujitokeza kuwasaidia chochote walichonacho ili kuwaongezea hamasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika Ligi Kuu inaayoendelea hivi sasa hapa nchini.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Shea Mohamed aliwashukuru wana-Mlandizi kwa uchache wao ambao wanathamini mchango wa timu hiyo, huku akiwaomba waendelee kujitokeza kuisaidi ili ifanye vizuri zaidi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...