Search This Blog

Monday, January 4, 2021

Makurunge wasafisha eneo la kujenga Sekondari


Na Omary Mngindo, Makurunge

WAKAZI wa Vitongoji vya Mkwajuni, Gezaulole, Mtoni, Kitame, Kifude na Kibaoni Kata ya Makurunge Jimbo la Bagamoyo Pwani, wameanza kusafisha eneo litalojengwa shule ya sekondari ya Kata hiyo.

Usafi huo ulioanzia kwa kutumia greda walilolikodi kwa shilingi milioni moja na laki nane kwa siku mbili, inatokana na michango iliyotolewa na viongozi wa serikali kwa niaba ya wananchi wa maeneo yao, hatua inayolenga kuwaondolea adha wanafunzi.

Wakizungumza na Waandishi wa habari eneo la tukio, Diwani wa Kata Hamisi Mbonde alisema hatua hiyo inalenga kuwaondolea adha wanafunzi wanaosafiri mpaka Fukayosi au Kata ya Magomeni kupata elimu, hali inayosababisha usumbufu mkubwa.

"Kwa kila siku mzazi au mlezi amalazimika kutumia zaidi ya shilingi elfu mbili kwa ajili ya nauli ya wanafunzi kwenda Fukayosi na kurudi, hali ambayo ni mzigo mkubwa ukizingatia kipato chao hakikidhi gharama hiyo," alisema Mbonde.

Aliongeza kwamba baada ya usafi huo wanataraji kuwajulisha wananchi wote katani hao kufika tayari kuanza kuchimba msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule hiyo, inayitaraji kuanza kupokea wanafunzi mwezi wa pili mwaka huu.

"Harakati hizi zinaungwa mkono kwa asilimia kubwa na Mbunge wetu Muharani Mkenge, ambaye alipokuwa kwenye ziara ya kushukuru hivi karibuni aliutaka uongozi wa Kata kumjulisha siku ya kuanza kuvhimba msingi ili nae aweze kuhudhulia," alisema Mbonde.

Alisema kwamba wanayo matofari zaidi ya elfu sita, nondo na vifaa vinavyohusiana na ujenzi, na kuwa matarajio yao ni kukimbizana na agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa la kuwataka viongozi kujenga shule mpya au vyumba vya kutosha ili kuwapokea wanafunzi wote wataofaulu.

Kwa upande wao Hamisi Mwanamkuta Ofisa Elimu Kata, Juma Ngwambi Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mkwajuni, Amani Mdoe Mwenyekiti Jumuia ya Wazazi Kata na Hussein Mwinyimvua Katibu wa Vitongoji cha Gezaule walisema kwamba wana-Makurunge wameupokea kwa moyo mmoja ujenzi huo.

"Wana-Makurunge wamehamasika sana kwani kwa miaka mingi vijana wetu walikuwa wanakwenda umbali mrefu kufuata masomo, wazazi walikuwa wanalazimika kutumia zaidi ya shilingi elfu mbili kwa ajili ya nauli na hela ya kula," alisema Mwinyimvua.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...