Majaji 2 wa kike wameripotiwa kupoteza maisha katika shambulizi la silaha kwenye gari katika mji mkuu wa Kabul, nchini Afghanistan.
Idara ya polisi ya Kabul ilitangaza kwamba majaji wa kike walishambuliwa na watu wasiojulikana kwenye eneo la Kale-i Fethullah katika mji mkuu.
Majaji hao wa 2 wa kike walifariki katika shambulizi hilo, na wengine 2 walijeruhiwa.
Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hadi kufikia sasa.

No comments:
Post a Comment