Search This Blog

Friday, January 1, 2021

KMC FC yaachana na wachezaji wake wawili


Wakati kipindi cha usajili wa dirisha dogo ukiendelea, KMC FC imeachana na wachezaji wake wawili ambao ni David Mwasa ambaye ameuzwa kwenda Mbeya City pamoja na Salim Aiyee kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba wake.

Salimu alijiunga na KMC  kwa mkataba wa miaka mwili akitokea Mwadui FC  ambapo ameitumikia Timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2021.

Kwa upande wa Mwasa ambaye alijiunga na KMC FC kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli, na hivyo kutumikia KMC FC kwa kipindi cha miezi sita kabla ya mkataba wake kumalizika Juni 2022.

KMC FC inawashukuru wachezaji hao kwa mchango mkubwa walioutoa wakati wa kitimiza majukumu yako na kwamba tunaimani kuwa watakwenda kufanya vizuri zaidi katika timu zao mpya wanaokwenda kuzitumia hivi  sasa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...