Search This Blog

Friday, January 1, 2021

Diwani kata ya Boay afunga mwaka kwa kuwakusanya pamoja Wananchi


Na John Walter-Boay, Babati

Bonanza la michezo la kufunga na kukaribisha mwaka mpya wa 2021 lililoandaliwa na Diwani wa kata ya Boay Babati mkoani Manyara  limefana na kuleta ushindani mkubwa kwa timu shiriki za mpira wa miguu.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika bonanza hilo Diwani wa kata ya Boay  Mheshimiwa  Samson Shamba Hilbajojo (CCM),  amesema Bonanza hilo la kufunga mwaka 2020 na kuukaribisha 2021 ni maalum kwa ajili ya  kurudisha shukrani kwa wananchi  wa kata hiyo na wote waliomuamini na kumpa nafasi ya kuwa diwani.

Hilbajojo amesema yeye kama mdau wa Michezo ataendelea kuendeleza michezo katika kata yake  ili kudumisha amani, umoja na upendo na pia wananchi kuwa na afya bora.

“Nitaendelea kuunga mkono suala la michezo na kusapoti kadiri inavyowezekana maana michezo ni afya na inajenga Undugu" amesema Hilbajojo.

Kwa upande wao washiriki wa Bonanza hilo wamemshukuru Diwani huyo kwa kufanikisha shughuli hiyo ambayo imewaweka karibu wananchi wa kata ya Boay na kata zingine jirani.

Mchezo uliowavutia wengi ni ule wa Wakongwe waliowahi kucheza mpira enzi za ujana wao ambapo walionyesha uwezo waliokuwa mkubwa katika kusakata soka.

Washindi katika Bonanza hilo kwa upande wa riadha Mita 100, wa kwanza ni Samweli Jacob na wa pili ni Abushehe Muhindi, mita 1500 Samweli Jacob alishika nafasi ya kwanza na ya pili kwa Abushehe Muhindi.

Kuvuta kamba Mshindi Big Boys kutoka Bondeni waliongoza.

Katika mpira wa miguu mshindi wa kwanza ni Kikilo Fc kutoka kondoa mkoani Dodoma waliokuja kama waalikwa, wa pili ni Chego Fc na ya tatu ni Bondeni Fc.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...