Search This Blog

Tuesday, January 12, 2021

Israel kujenga nyumba 850 katika makazi ya Wapalestina


Imearifiwa kuwa Israeli itajenga kinyume cha sheria nyumba 850 zaidi kwa walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi uliokaliwa kimabavu.

Mamlaka ya Israel imeidhinisha uamuzi wa kujenga makazi mengine 850 katika Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya walowezi wa Kiyahudi wiki ijayo.

Taarifa hii ni kulingana na Shirika la Utangazaji la Umma la Israel KAN.

Katika ripoti hiyo, imebainika kuwa Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz aliagiza Baraza la Mipango ya Juu la Kitengo cha Utawala wa Kiraia ndani ya Kitengo cha Uratibu wa Shughuli za Serikali (COGAT) kujenga nyumba zaidi katika Wilaya za Palestina zilizokaliwa kimabavu na Wayahudi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kutoka mamlaka ya Israel juu ya suala hilo.

Inafahamika kuwa Israel imechukua hatua kama hiyo muda mfupi kabla ya rais mpya Joe Biden kuchukua wadhifa wake.

Kwa uungwaji mkono usio na masharti wa Rais wa Marekani Donald Trump, mamlaka ya Israeli imeharakisha shughuli za kujenga na kupanua makazi ya Wayahudi kabla ya Biden kuanza kazi, ambaye alionyesha kupinga kwao ujenzi haramu wa nyumba katika Ukingo wa Magharibi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...