Search This Blog

Tuesday, January 12, 2021

Serikali mpya imeundwa kufuatia uchaguzi wa urais uliofanyika Burkina Faso


Serikali mpya imeundwa kufuatia uchaguzi wa urais uliofanyika Burkina Faso tarehe 22 Novemba.

Waziri Mkuu Christophe Marie Joseph Dabire ametangaza kuunda serikali mpya ya watu 33, wakiwemo manaibu waziri 7 na waziri aliye chini ya rais.

Kiongozi wa zamani wa upinzani Zephirin Diabre, ambaye pia ni mgombea wa urais, amechukua nafasi katika baraza la mawaziri.

Rais Roch Marc Christian Kabore, ambaye alizingatia mchakato wa upatanisho wa kitaifa wakati wa kampeni zake za uchaguzi, alisema katika ujumbe wake waTwitter kwamba Waziri Mkuu Dabire aliunda baraza jipya la mawaziri kwa kuzingatia ahadi hii.

Dabire pia alikuwa waziri mkuu katika serikali iliyopita.

Mawaziri wengi wamerudi katika baraza jipya la mawaziri.

Uchaguzi wa Rais ulifanyika Burkina Faso tarehe 22 Novemba.

Rais Kabore wa sasa amechaguliwa kwa muhula wake wa pili, kwa kupata asilimia 57.74 ya kura.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...