Rais wa India Ram Nath Kovind, ametangaza kuwa atatuma wanajeshi zaidi kwenye mpaka wa India na China.
Kulingana na taarifa ya South China Morning Post, Rais wa India Kovind aliripoti kuwa wanajeshi zaidi wametumwa katika eneo la mpaka wa "De facto Control" ili kulinda uhuru wa nchi hiyo.
Akizungumza katika Bunge, Kovind alifahamisha kuwa kikosi cha ziada kilitumwa kulinda uhuru wa India katika eneo la mpaka wa "De facto Control", na kusema,
"Serikali yangu imejitolea kikamilifu kulinda masilahi ya taifa."
Mpaka usiokuwa wa wazi ambao umezungukwa na Milima ya Himalaya kati ya nchi hizo mbili umekuwa chanzo cha mizozo ya kati ya China na India.
Mpaka huo wa urefu wa kilomita 3,500 wenye mito, maziwa na kilele cha theluji mara nyingi husababisha mapigano kati ya pande hizi mbili.
Utawala wa Beijing unadai kilomita za mraba 90,000 za ardhi katika jimbo la India la Arunachal Pradesh, ambalo linaitwa "Tibet Kusini", wakati New Delhi nayo inadai kuwa kilomita za mraba 38,000 za ardhi inayofunika eneo la Aksay China zimevamia na China.
Wakati pande zote zikishindwa kutatua mizozo yao licha ya mazungumzo ya muda mrefu, mvutano kati ya nchi hizo mbili uliongezeka mnamo 2017 baada ya China kujaribu kupanua barabara ya mpakani katika eneo hilo.

No comments:
Post a Comment