Search This Blog

Friday, January 29, 2021

Waziri Mwambe akutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Dangote na wazalishaji wa Sukari Nchini


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini.

Akizungumza na  wazalishaji hao leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe.Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija  kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.

''Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi''amesema Mhe.Mwambe.

Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili  kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji zaidi nchini .

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...