Search This Blog

Wednesday, January 20, 2021

Hatua kali za kuzuia janga la corona Ujerumani zimerefushwa hadi Februari 14


Ujerumani imerefusha hadi Februari 14 hatua kali za kuzuia janga la corona na kuweka sheria kali za uvaaji barakoa maalum kwa watu wanaoingia madukani na kwenye vyombo vya usafiri.

 Kansela Angela Merkel ameonya kuwa nchi lazima ichukue "hatua sasa" ili kuzuia kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Covid-19. 

Waraka ulioandaliwa na serikali ya Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo 16 umeelezea wiki zijazo kuwa "muhimu", ukitaja kitisho kinachosababishwa na aina mpya ya virusi vya corona ambavyo vinaambukiza kwa kasi kulikuwa kile cha awali. 

Merkel pia amedokeza kuzinduliwa kwa utoaji chanjo ya corona Ujerumani, akisema kufikia mwisho wa msimu wa joto, chanjo hiyo inapaswa kutolewa kwa kila mkazi. 

Zaidi ya watu milioni 2.05 wameambukizwa corona Ujerumani mpaka sasa huku 47,622 wakifariki dunia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...