Search This Blog

Wednesday, January 20, 2021

Manispaa Mtwara Mikindani yadai bilioni 1.7 ya kodi ya ardhi

 



Na Faruku Ngonyani, Mtwara

Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani iliyopo Mkoani Mtwara inadai jumla sh bilioni 1.7 kwa wadawaiwa sugu wa kodi kutoka taasisi Zaidi 43 za serikali na Zaidi taasisi 30 za watu binafsi.

Akuzungumza kwenye kikao kilichowajumuisha wadiwa hao Mkuu wa wa Wilaya ya Mtwara Dunstani Kyobya amewataka kulipa fedha hizo kwa wakati ili ziende kutumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

Kikoa hiko kilifanyika katika ukumbi wa Benjamini Wiliam Mkapa uliopo chuo cha ualimu cha TTC kilichopo kata ya shangani Manispaa Mtwara Mikndani.

Mkuu wa Wilaya Kyobya ametoa wito kwa Halmashuri ya Manispaa Mtwara Mikindani kuhakikisha wanarekebisha mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya ardhi ili kuondoa sitomfahamu kwa baadhi ya wananchi wanapokuwa wanalipa kodi hizo.

Nae Mkurugnzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani Kanali Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa kwa wadaiwa hao changamoto kubwa ipo kwa taasisi kwa kuwa hela nyingi zipo kwa upande wao huku taasisi moja inadiwa Zaidi ya milioni mia moja.

Wadaiwa hao wametakiwa kuanza kulipa madeni yao kuanzia tarehe 30 januari 2021.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...