Search This Blog

Wednesday, December 16, 2020

'Zaidi ya watoto milioni 2' wakosa msaada Tigray


Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watoto milioni mbili katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia wamekatizwa na misaada ya kibinadamu huku ghasia zikiendelea.

Licha ya makubaliano ya yaliyofikiwa na serikali ya Ethiopia, mashirika ya kutoa misaada yanalalamikia kuzuiliwa kuingia Tigray ambako vikosi vya serikali vimekuwa vikikabiliana na wapiganaji wa Tigray Liberation Front kuanzia mapema mwezi Novemba.

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, linahofia kadri linavyochelewa kuwafikia watoto katika eneo holi ndivyo hali yao wanaohitaji msaada wa dharura itaendelea kuzorota.

Mapema mwezi huu wanajeshi waliwaelekezea marisasi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Tigray.

Serikali imesema wafanyakazi wa UN hawakuwa na ruhusa ya kusafiri katika eneo hilo na kuwalaumu kwa kuvuka vizuizi vilivyowekwa barabarani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...