Mevlüt Çavuşoğlu alitoa taarifa kwenye Twitter na kuarifu kupokewa na kukaribiswa na Rais Widodo nchini Indonesia, wakati alipotekeleza ziara yake rasmi.
Akiripoti kuwasilisha salamu za Rais Recep Tayyip Erdoğan kwa Widodo, Çavuşoğlu alisema,
"Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mkakati wa kiwango cha juu utafanyika mwaka ujao wakati wa ziara ya Rais wetu. Mahusiano na mshirika wetu muhimu, Indonesia ambayo pia ni nchi rafiki na ndugu katika Asia ya Kusini-Mashariki yanaendelea katika nyanja zote."
Kulingana na taarifa kutoka vyanzo vya kidiplomasia, Çavuşoğlu baadaye alikutana na Waziri wa Ulinzi Subianto. Çavuşoğlu alikaribishwa kwa sherehe ya kijeshi, na baadaye akafanya mkutano na wajumbe na Wizara ya Ulinzi ya Indonesia.
Akikumbushia ziara 5 za Uturuki alizofanya Subianto ndani ya mwaka jana, Çavuşoğlu alisema,
"Tutaimarisha zaidi ushirikiano wetu katika sekta ya ulinzi. Tunataka kusaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi hivi karibuni."

No comments:
Post a Comment