Search This Blog

Tuesday, December 22, 2020

Putin na Abbas wajadili masuala ya Palestina


Rais wa Urusi Vladimir Putin alijadili suala la Palestina kwa njia ya simu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Kremlin, iliarifiwa kwamba Putin aliwasiliana na Abbas kwa njia ya simu.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili masuala ya uhusiano na ushirikiano kati ya nchi mbili na juhudi za kupambana na janga la virusi vya corona (Covid-19).

Katika mazungumzo hayo ambayo pia yalijadili suala la Mashariki ya Kati, Putin alithibitisha kuwa Urusi iko tayari kuunga mkono suluhisho la haki na la kudumu kuhusu mzozo wa Palestina katika siku zijazo.

Viongozi hao wawili pia walikubaliana kuendeleza mawasiliano katika nyanja mbalimbali.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...