Search This Blog

Friday, December 25, 2020

Watu wanne washikiliwa kwa tuhuma za Qnet

 


Jeshi la Polisi wilayani hapa Mkoa wa Mara, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujihusisha na mtandao wa Kampuni ya Qnet na kutapeli watu.


Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Vicent Naano alisema hayo mjini hapa jana na kuongeza kuwa watu hao wanashikiliwa baada ya operesheni kufanywa na vyombo vya dola.


Alisema polisi walibaini watu wanaojihusisha na mtandao huo na jumla ya watu 25 walikamatwa baada ya uchunguzi.


Hata hivyo, Dk Naano hakuwa tayari kutaja majina ya watuhumiwa hao ingawa alisema faili kuhusu watu hao limepelekwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali kwa ajili ya taratibu za kufikishwa mahakamani.


Alisema uchunguzi umebaini kuwa watu wengi mjini Musoma wametapeliwa na mtandao huo ikiwamo familia moja ya mstaafu wa Serikali ambayo ilitapeliwa Sh15 milioni ingawa hakuwa tayari kutaja jina la mstaafu huyo.


“Huyu mama alikuwa mtumishi pale manispaa, baada ya kustaafu alipeleka Sh5 milioni Qnet kisha binti yake akapeleka Sh5 milioni, kabla huyu mama hajampa kijana wake mwingine Sh5 milioni fedha ambazo hadi sasa hawajarudishiwa,” alisema Dk Naano.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...