Kiongozi wa kanisa katoloki duniani Papa Francis ametoa wito kwa viongozi duniani kuhakikisha chanjo ya corona inawafikia watu wote.
Katika ujumbe wake wa siku ya Krismasi uliyowasilishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza, Papa alitoa onyo dhidi ya kuweka "kuta" katika matibabu.
Janga la corona mwaka huu lilimaanisha ujumbe wa kila mwaka wa Urbi et Orbi haukuwasilishwa kutoka kwenye roshani ya kwenye St Peter Basilica kwa umati mkubwa wa watu, kama jadi.
Badala yake Papa alizungumza katika chuma kimoja ndani ya Vatican.
Onyo la Papa Francis linakuja wakati kumekuwa na hofu nchi zilizo na uwezo mkubwa zinanunua dozi nyingi za chanjo hali ambayo itakuwa na athari kwa nchi masikini.
"Naomba Mwana wa Mungu awaguse viongozi wa kisiasa na mataifa katika ushirikiano wa kimataifa, kuanzia kwa huduma ya afya, ili kila mtu apate chanjo na tiba," alisema.
"Changamoto inayotukabili haijui mipaka, hatuwezi kuweka kuta. Sote tuko katika dau moja."
Papa amesema athari za mzozo wa kiafya zinaashiria umuhimu wa kuwa ulimwengu kuwa kitu kimoja kuliko ilivyokuwa hapo awali.

No comments:
Post a Comment