Search This Blog

Sunday, December 27, 2020

Watu 7 wauawa nchini China baada ya kushambuliwa kwa kisu

 


Watu wasiopungua saba wamekufa na wengine 7 kujeruhiwa katika shambulizi la kisu lililotokea leo kaskazini mashariki ya China. 

Kituo cha habari cha taifa kimeripoti kuwa shambulzii hilo kwenye mji wa Kaiyuan katika jimbo la Liaonig limetokea nje ya jumba lenye Sauna na dimbwi la kuogelea. 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mtuhumiwa, amekamatwa na ametambuliwa kwa jina moja la Yang, lakini hata hivyo nia ya shambulio hilo bado haijabainika. 

Kwa mujibu wa sheria ya China uuzaji na umiliki wa silaha hauruhusiwi, na hivyo mashambulizi mengi hufanywa kwa kutumia visu au vifaa vya kulipuka vilivyotengenezwa nyumbani. 

Washambuliaji waliowahi kufanya matendo hayo hapo awali wametajwa kuwa ni wagonjwa wa akili au watu wenye hasira na chuki dhidi ya jamii.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...