Mataifa ya Umoja wa Ulaya leo yameanza kwa pamoja kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa makundi ya watu walio kwenye hatari hatua inayoleta faraja kwenye mapambano dhidi ya mzozo huo wa kiafya kuwahi kushuhudiwa kwenye kanda hiyo.
Dozi za chanjo zimeanza kutolewa mapema leo asubuhi kwa wafanyakazi wa huduma za afya, wazee pamoja na wanasiasa kadhaa kwa lengo la kuuhakikishia umma kuwa chanjo hiyo ni salama.
Waziri Mkuu wa wa Jamhuri ya Czech Andrej Babis amepatiwa chanjo kwenye mji mkuu, Prague, na kuwaambia raia wa nchi hiyo hawana sababu ya kuwa na hofu.
Akizungumza kwenye hospitali moja mjini Roma, Waziri wa Afya wa Italia Roberto Speranza amesifu mpango wa pamoja ya Umoja wa Ulaya katika zoezi la kutoa chanjo lakini amewataka wakaazi wa kanda hiyo kuendelea kuchukua tahadhari.

No comments:
Post a Comment