Search This Blog

Friday, December 18, 2020

Watu 15 wapoteza maisha kwenye shambulizi la bomu nchini Afghanistan


Raia 15 wameripotiwa kuuawa kwenye shambulizi la bomu lililotekelezwa kwenye wakati ya shughuli ya hafla iliyoandaliwa katika mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Tarık Aryen, alitoa taarifa kwa waandishi wa habari na kusema kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa wakati wa hafla ya hatim ya Quran iliyoandaliwa katika kijiji cha Agujan wilayani Geylan mkoani Ghazni, ambapo  pikipiki yenye mabomu 3 ilitumika.

Aryen alibainisha kuwa raia 15 walipoteza maisha na wengine 20 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Hakuna yeyote aliyedaiwa kuhusika na shambulizi hilo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...