Na Faruku Ngonyani,Mtwara
Wananchi wa kata ya Nakahako, Mikumbi na Chilangala Zilizopo Halmashauri ya Wilaya Newala Mkoani Mtwara wamelalamikia kutokamilika kwa wakati mradi wa maji lukohe na mnima miyuyu ulioanza kutekelenzwa 2018 na mamlaka ya usambazaji maji na usafi wa mazingira RUWASA ambapo mradi huo ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi tisa tangu kuanza kwake
Wakizungumza katika kongamano la ushawishi na utetezi katika kuziangazia changamoto za miradi ya Maji Lukohe na mnima Miyuyu lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la NEHIA kupitia Mradi wa Medi kwa Maendeleo vijijini wamesema hawatarajii kuona Maji yakitoka katika maeneo yao kutokana na uwepo wa changamoto hiyo kwa muda mrefu
Kwaupande wao Madiwani kata hizo wametoa Rai ya kuchukua hatua kwa wakandarasi na kuchunguzwa waliotekeleza mradi huo kutokana na kukamilika na kushindwa kutoa maji
Aidha wamesema Mradi huo wa Lukohe na Mnima Miyuyu kwa kata ya Mikumbi umegharimu kiasi cha shl bil 5.9 kwa kata ya Chilangala bil5.9 na Nahahako bil 2.29 ambapo wakandarasi wamehitimisha lakini hautoi maji kutokana na changamoto zinanazojitokeza
Aidha madiwani hao wameliomba shirika la NEHIA kuendelea kufuatilia mradi huo ili waweze kuwasaidia.
Akieleza kuhusiana na mradi huo kaimu Meneja wa mamlaka ya usambazaji Maji na usafi wa Mazingira mjini na vijijini RUWASA ENG Juma Hassani Musaa ameagidi kuwa na kusema kuwa ifikapo Disemba 31 mwaka huu utakuwa umekamilika na wananchi watapata maji
Kwa upande wake mwenzeshaji kutoka shirika NEHIA Peter Kibehi ameahidi kuendelea kufuatilia miradi hiyo maji.

No comments:
Post a Comment