Na John Walter-Manyara
Mwenyekiti wa Kamati ya ushauri ya mkoa wa Manyara ambaye ndiye mkuu wa mkoa Joseph Mkirikiti amewaomba wabunge wa mkoa huo kuwashawishi Wabunge wenzao kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya taifa ya Tarangire.
Wito huo ameutoa wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika mkoani hapo ambapo amesema ombi hilo likifanikiwa litasaidia kwa kiasi kikubwa kuutangaza mkoa wa Manyara na kuongeza mapato kwenye sekta hiyo ya Utalii na ndani ya mkoa.
Mkoa wa Manyara unajumla ya Wabunge kumi, Saba waliochaguliwa kwenye majimbo na wengine watatu wa viti maalum.
Mkoa wa Manyara mbali na kuwa na hifadhi kubwa za Taifa Tarangire na Manyara lakini pia una vivutio vingi vya asili kama Kisima cha Mungu, Maji moto, Kichuguu kinachonesa, mlima Kwaraa na Mlima Hanang.
Aidha Mkirikiti amewataka wadau wa maendeleo nchini kuwekeza kwenye Wilaya za Mkoa huo kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali za kiuchumi.
Amesema mkoa huo una fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, madini, uvuvi, utalii na nyingine hivyo ni muda wa kuchangamkia fursa hizo kwenye mkoa huo wa tatu kwa ukubwa nchini.

No comments:
Post a Comment