Search This Blog

Friday, December 25, 2020

Mati Super Brand watoa msaada kituo cha watoto yatima cha Hossana

 


Na John Walter-Babati

Uongozi wa kampuni ya Mati Super Brand Ltd wilayani Babati mkoani Manyara wakiongozwa na mkurugenzi wa kampuni David Mulokozi, wamefanya tendo la huruma kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Watoto Yatima cha  Hossana Home care Foundation kilichopo kijiji cha Managha kata ya Singe mjini Babati.


Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada kituoni hapo Desemba 24, 2020  Mkurugenzi wa Mati Super Brand David Mulokozi  alisema wamefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo inayojihusisha na uzaishaji wa pombe Kali na bidhaa nyingine kusaidia kundi hilo lenye uhitaji katika jamii ili waweze kufurahia siku kuu ya Krismas.


Miongoni mwa vitu walivyopatiwa watoto hao ni pamoja na mchele, maharage, Mahindi, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi, dagaa, majani ya chai, juisi, Viatu, nguo, madaftari na kalamu, sabuni na vifaa vya usafi.


Kwa upande wa uongozi wa Kituo hicho, waliushukuru uongozi wa kampuni hiyo kwa kutambua uhitaji wa watoto wa Kituo hicho na kuomba makundi mengine kutosita kujitokeza kusaidia watoto hao.


Kituo hicho kilianzishwa mnamo mwaka 2019.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...