Search This Blog

Thursday, December 17, 2020

Ujerumani imepanga kuanza chanjo ya virusi vya corona Desemba 27


Waziri wa Afya wa Ujerumani, Jens Spahn amesema Ujerumani imepanga kuanza kampeni ya utoaji chanjo ya virusi vya corona Desemba 27, huku mataifa yote 27 ya Umoja wa Ulaya yakiwa na lengo la kuanza siku hiyohiyo. 

Katika taarifa yake Spahn amesema pale itakaporidhiwa wezee ambao wanaishi katika vituo vya kuwatunzia wazee ndio watakaokuwa wa kwanza kupata chanjo hiyo ya Pfizer-BioNTech. 

Waziri huyo wa afya ametoa taarifa hiyo baada ya kufanya mkutano na maafisa wa afya kutoka katika majimbo 16 ya Ujerumani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...