Watuhumiwa 14 walioshitakwa kwa kosa kupanga shambulizi la kigaidi kwenye ofisi za jarida la tashtiti la Charlie Hebdo la Januari 2015 na eneo lingine la duka kubwa la kiyahudi nchini Ufaransa wamekutwa na hatia.
Kwa mujibu wa mahakama miongoni mwao watahukumiwa vifungo vya kati ya miaka 4 hadi maisha.
Miongoni mwa waliopandishwa kizimbani ni pamoja na mshtakiwa mkuu ni Ali Riza Polat, ambaye anatuhumiwa kwa kuyapanga mashambulizi hayo ambae amehukumiwa miaka 30, vilevile kijana wa umri wa miaka 35, mwenye asili ya Kifaransa na Kituruki aliyekutwa na hatia ya kusaidia na kuchochea uhalifu wenye dhamira ya kigaidi ikiwa na miongoni na mashitaka mengine pia amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.
Wote kwa pamoja wanahusishwa na mfululizo wa mshambulizi ya 2015 ya mjini Paris ambapo watu 17 waliuwawa.
No comments:
Post a Comment