Search This Blog

Friday, December 25, 2020

Uchaguzi mkuu waahirishwa nchini Ethiopia


Uchaguzi mkuu ulioahirishwa nchini Ethiopia kutokana na janga la virusi vya corona (Covid-19), umepangwa kufanyika tarehe 5 Juni, 2021.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani ya nchi, Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (NEBE)  ilitangaza kuwa uamuzi huu ulichukuliwa baada ya mashauriano na vyama vya siasa.

Tume hiyo imearifu kwamba uchaguzi mkuu ulioahirishwa utafanyika tarehe 5 mwezi Juni, ingawa tarehe hiyo pia inaweza kubadilika kulingana na hali ya nchi itakavyokuwa.

Katika taarifa hiyo pia iliarifiwa kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu yataweza kutangazwa kati ya tarehe 6-28 Juni.

Nchi ya Ethiopia ilichukuwa uamuzi wa kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Agosti kutokana na janga la Covid-19.

Baadhi ya vyama vya upinzani vimeitaka serikali kugawana madaraka endapo uchaguzi hautofanyika.

Nchi ya Ethiopia ambayo ina muundo wa mabunge mawili,  ina viti 112 katika Bunge Kuu la serikali na viti 547 katika Baraza la Wawakilishi la Wananchi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...