Search This Blog

Friday, December 25, 2020

Faini kubwa kwa watoaji taarifa za uwongo Urusi


Nchi ya Urusi itaanza kutoa hukumu na adhabu kali kwa wahusika wa utoaji wa taarifa na madai ya uwongo yasiyokuwa ya msingi mitandaoni.

Kfuatia sheria iliyopitishwa katika bunge la mrengo wa chini nchini Urusi, faini ya fedha itatozwa kwa wahusika wa utoaji taarifa na madai ya uwongo kwenye mitandao ya kijamii na pia huweza kugeuzwa kuwa hukumu ya kifungo cha gerezani.

Hivyo basi, mmiliki wa akaunti ya mtandao wa kijamii ambao utachapisha au kusambaza habari za kashfa na zisizo na msingi juu ya maafisa wa serikali, atatozwa faini ya takriban dola 27,000.

Wale ambao hawatoweza kulipa faini hiyo, watahukumiwa kifungo cha hadi miaka 3 gerezani.

Kwa taarifa za uwongo juu ya afya ya mtu, hukumu yake itakuwa ni faini ya dola 40,000 au kifungo cha hadi miaka 4 gerezani.

Wahalifu wa unyanyasaji wa kijinsia na kashfa za mitandaoni wanatarajiwa kutozwa faini ya dola 67,000 au kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 5 gerezani.

Hapo awali, uhalifu wa aina hii pia ulikuwa ukitozwa faini.

Kwa sasa sheria hiyo iliyopitishwa katika bunge kuu iko kwenye meza ya Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Ikiwa itaidhinishwa, utekelezaji utaanza rasmi kuanzia mwaka mpya.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...