Search This Blog

Thursday, December 17, 2020

Tanzania Redcross Society wajaza nafasi za uongozi Manyara


Na John Walter-Manyara

Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania (Tanzania Redcross Society) Mkoa wa Manyara, kimekamilisha kujaza safu za uongozi nafasi mbalimbali kutumikia wananchi na shirika hilo kwa miaka mitano ijayo.

Waliojaza nafasi hizo ni Theresia Chales Makamu wa Mwenyekiti, Ernest Mbuta Mratibu, Benard Laiza Mweka hazina, Haruni Mvungi meneja wa miradi, Sinda Sungwa mipango na maendeleo,

Wengine ni Jacob Kilitory Mollel mwenyekiti wa vijana, Eng Elipid Tesha mjumbe wa kuteuliwa na kitengo cha Habari na Maafa ni Mohamed Hamad.

Mkutano mkuu wa shirika umefanyikia mjini Babati, chini ya mwenyekiti wa Tanzania Redcross Mkoa wa Manyara, Wakili Moses Basila, ambaye alitaja idadi ya nafasi zilizokuwa wazi na ambazo zimejazwa na viongozi kwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.

Wakili Basila alisema kupatikana kwa viongozi hao kutatoa mwelekeo wa shirika hilo kutekeleza mipango yake ya miaka mitano ambayo itakuwa na tija kubwa kwa shirika na kwa wananchi mkoani humo.

Ameyataja malengo ya TRCS Manyara kuhakikisha shirika linakuwa na Ofisi ya Mkoa, kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato, kuongeza idadi ya wanachama wapya elfu 33,000 kwa miaka mitano kama lilivyo lengo la Taifa kuongeza wanachama wapya mil 1,00,000.

Malengo mengine ni kuwa na miradi mipya na kusimamia kikamilifu iliyopo chini ya wahisani ili kuleta tija, kuwa na vikundi vinavyozalisha ndani ya matawi pamoja na kuimarisha baraza la vijana.

Kwa upande wake Theresia Chales aliyechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Tanzania Redcross Society Mkoa wa Manyara, aliahidi wajumbe wa mkutano Mkuu kuwa atahakikisha anatimiza wajibu wake kama ilivyo katika kanuni saba za Redcross.

“Kuchaguliwa ni jambo moja, utekelezaji ni jambo lingine…nitakuwa na jukumu kubwa kuhakikisha nashirikiana na wenzangu kufikia malengo ya Tanzania Redcross ambayo ni kupunguza au kuondoa maumivu kwa wahanga”

Christopher Nzala mwezeshaji wa mafunzo kwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa Tanzania Redcross alisema, Redcross ni kisaidizi cha Serikali kutimiza majukumu yake kuhudumia wananchi ambapo alitaja kanuni saba za Redcross kuwa ni pamoja pamoja na Ubinadamu,Uadilifu, Uhuru, Kujitolea, Umoja na Hadhi sawa.

Alisema mwanachama akifahamu kanuni hizo atafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu mkubwa bila mawaa huku akiwataka kuzingatia kanuni ya tano, kujitolea ambayo ndio nguzo kuu ya Redcross katika kuwatumikia wananchi.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...