Rais wa Urusi Vladimir Putin, amempongeza Joe Biden, ambaye aliidhinishwa rasmi kama Rais mpya wa Marekani.
Kamati ya Uchaguzi ya Marekani imempitisha rasmi Joe Biden kuwa Rais wa 46 wa nchi hiyo.
Shirika la habari la Urusi la Ria lilitangaza kuwa Putin alimpongeza Biden.
Kulingana na matokeo ya uchaguzi uliofanyika Novemba 3 nchini Marekani, Joe Biden alishinda kwa kupata wajumbe 306 dhidi ya Trump aliyepata wajumbe 232.

No comments:
Post a Comment