Mazungumzo ya kibiashara ya baada ya Uingereza kujiondoa katika umoja wa Ulaya-Brexit bado yamekuwa katika mkwamo na leo kuwa katika kitisho cha kushindwa kabisa, wakati pande zote zikijiburuza katika maafikiano kuhusu maeneo ya hazina ya uvuvi ya Uingereza.
Pande zote mbili bado zinaonekana kutaka kila upande ulegeze masharti dhidi ya mwingine.
Bunge la Umoja wa Ulaya lililisema kuwa muda wa mwisho wa kupatikana mkataba unapaswa kuwa usiku wa leo Jumapili, ili kuwezesha mkataba huo kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka ambapo Uingereza inapaswa kuondoka katika soko la pamoja la Umoja wa Ulaya.

No comments:
Post a Comment