Idadi ya waliokufa kutokana na kimbunga kikali, Yasa cha juma lililopia kilicholikumba eneo la taifa lililo katika bahari ya Pasafik, Fiji imeongezeka na kufikia watu wanee, huku mmoja hajulikani alipo hadi sasa.
Mkurugenzi wa kitengo kinachohusika na majanga cha taifa hilo, Vasiti Soko aliwaambia waandishi wa habari kwamba takribani watu 7,731 wapo katika vituo vya uokozi 183 vya maeneo tofauti ya kisiwa hicho.
Kimbunga hicho kilichotokea Alhamis kiliyakumba maeneo ya mji mkuu wa Suva, na eneo la utalii la kisiwa hicho Nadi na Viti Levu, na athari zake zinaendelea kushuhudiwa hadi hivi sasa.
Soko amesema misaada ya kiutu inayotolewa na kikosi cha jeshi cha taifa hilo inafikishwa katika maeneo husika leo hii.

No comments:
Post a Comment